Timu ya taifa ya Tanzania chini ya
umri wa miaka 17 imeyaaga mashindano ya mataifa ya Afrika ya vijana chini ya
umri wa miaka 17 baada ya kukubali
kipigo cha goli 1- 0 toka kwa Niger.
Tunaweza kusema bahati haikuwa kwa
Tanzania ambao muda mwingi walionekana kucheza kwa kujiamini na kushambulia
mara kwa mara huku Niger wao wakicheza kwa tahadhari na kujiangusha angusha ili
muda uende na kutumia mipira mirefu kwa kushtukiza.
Goli pekee katika mchezo huo
limefungwa na Ibrahim baada ya mpira ambao golikipa wa Tanzania alidhani umetoka
kurudishwa ndani na kumkuta mfungaji alieiwezesha timu yake kutinga nusu
fainali katika dakika ya 42.
Tanzania sasa inarudi nyumbani na
ndoto zake kwenda India kombe la Dunia zimeishia hapo.
timu ya Tanzania imelingana pointi na Niger, ila Niger wanapata faida ya kuifunga Tanzania, na hivyo kusonga mbele.
timu ya Tanzania imelingana pointi na Niger, ila Niger wanapata faida ya kuifunga Tanzania, na hivyo kusonga mbele.
Vijana wamejitahidi ila bahati
haikuwa upande wao.
Kwa upande wa mechi nyingine ya
kundi B Mali imetoa onyo kali baada ya kuifunga Angola 6 – 1.
Millionaire Ads
0 Comment untuk " Tanzania 0 - 1 Niger, Serengeti Boys out CAFU17"