Timu anaitumikia mtanzania Farid
Mussa huenda ikapata bahati ya kucheza ligi kuu ya Hispania msimu ujao kama
itafanikiwa kumalizwa katika nafasi za timu sita za juu.
Utaratibu wa Hispania ni kuwa timu
mbili za mwanzo zinapanda moja kwa moja ligi kuu’LaLiga’ na timu nne zilizobaki
yaani nafasi ya 3 mpaka ya 6 zinacheza ‘PlayOff’ili kupata timu moja ambayo
itaungana na mbili za juu kupanda daraja.
Ligi daraja la kwanza nchini Hispania
inashirikisha jumla ya timu 22, hivyo kila timu kwa msimu inatakiwa icheze mara
42.
Mpaka sasa ni raundi ya 39 kwa Tenerife
na timu nyingine nyingi Msimamo upo chini, Tenerife imejikusanyia pointi 60
katika nafasi ya nne nyuma ya vinara Levante wenye pointi 80 kwa michezo 39,
wakifuatiwa na Girona wenye pointi 69 baada ya michezo 39 na ya tatu ni Getafe
yenye pointi 64.
Katika michezo mitatu iliyobaki
uwezekano wa kuingia nafasi ya pili haupo kwani tayari Girona ina pointi 69
ambazo endapo Tenerife itashinda michezo yote itafika.
Nafasi pekee kwa Tenerife ni kuwania
mojawapo kati ya nafasi 6 za mwanzo zilizobaki ili badae kucheza playoff na
wakifanikiwa watakuwa wamepanda ligi kuu ya Hispania ‘LaLiga ’
Ndio maana tunasema Tenerife mguu
ndani, mguu nje LaLiga.
Angalia Msimamo wa ligi yao hapo
chini
0 Comment untuk "Club Deportivo Tenerife ya Farid Mussa mguu ndani mguu nje Laliga 2017/2018"