Ligi kuu Tanzania Bara 2016/17
imefikia patamu ikiwa 95% timu zote zimebakisha mchezo mmoja kivumbi kipo
kuwania ubingwa na timu zinazotakiwa kushuka daraja.
Ubingwa ni mchuano wa mahasimu wa
soka la bongo simba na Yanga ambapo mpaka leo hii Yanga na Simba wamefungana
pointi ila Yanga anaongoza kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, ila
Yanga ina mchezo mmoja pungufu ya Simba
Simba imebakisha mchezo mmoja tu
ambao utapigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa may 20 dhidi ya Mwadui
Yanga imebakisha michezo miwili
mmoja dhidi ya toto jumane may 16 Uwanja wa Taifa wakati mchezo wao wa mwisho
utafanyika jijini Mwanza dhidi ya Mbao FC may 20.
Uhondo upo zaidi kuwania kubaki ligi
kuu baada ya Matokeo ya leo kutoa matumani kwa baadhi ya timu, Majimaji wamejifikishia
pointi 32 na kujitengenzea mazingira mazuri ya kubaki endapo tu wataifunga timu
ya Mbeya city may 20 huko Songea, Mbeya city yenyewe ina pointi 33.
Toto wao watamaliza ligi huko
Manungu kukabiliana na timu ya Mtibwa ambayo itataka kulinda heshima tu kwani
haitaki ubingwa wala haishuki daraja.
Ndana wao leo wamepigwa 2 -1 na
Prisons hivyo kusalia na ponti zao 30 na watamaliza na timu ambayo ishashuka
daraja ya JKT Ruvu katika dimba la Nangwanda mkoa mtwara ikishinda ponti 33.
Timu ya AfricanLyon kesho jumapili inacheza mchezo wake wa 29 na
Ruvu Shooting huku ikwa na pointi 31ambazo
si salama hata kidogo, wakati ruvu shooting nae akiwa na pointi 33.
Mechi ya mwisho may 20 African Lyon itakuwa
na kibarua kizito mbele ya Prisons,
Mbio za ufungaji bora zinazidi
kumkalia vizuri mshambuliaji wa timu ya Yanga Simon Msuva kwa kufikisha goli 14
huku Mbaraka Yusuf, Obrey Chirwa na Mussa wakimkaribia kwa ukaribu
MATOKEO YA LEO NI KAMA IFUATAVYO
Yanga 2 - 1 Mbeya City
Prisons 2-1 Ndanda
Mtibwa 4-2 Mwadui
JKT 0-1 Majimaji
Kagera 2-1 Mbao FC
0 Comment untuk "Yanga 2 - 1 Mbeya City, Msuva akaribia kiatu cha dhahabu, yanga yaukaribia ubingwa, Majimaji yajiweka mahali salama kidogo"