Golikipa wa timu ya Taifa ya Chile
ambae pia ndie mlinda mlango wa timu ya Manchester City ya England jana usiku
aliibuka shujaa wa mchezo wa nusu fainali baada ya kuipeleka timu yake ya Chile
Fainali ya kombe la Mabara.
Mchezo wa jana ulikuwa mgumu kwa
kila upande na kupelekea dakika 90 kuisha bila goli lolote kwa kila timu.
Dakika 120 pia ziliisha bila timu
yoyote kupata goli, na ndipo sheria ya mikwaju ya penati ilipoamuliwa na
kupigwa.
Ushujaa wa Bravo ulionekana muda huu
wa penati baada ya kuondoa mikwaju mitatu ya mwanzo ya Ureno huku Chile
wakipata mikwaju yote ya mwanzo.
Bravo aliokoa mikwaju ya Ricardo
Quaresma, Moutinho na Nanj huku chile wakifunga kupitia kwa Vidal,Sanchez na
Aranguiz.
Kwa mantiki hii Chile wametinga
fainali ya michuano hii wakimsubiri mshindi katika mchezo wa leo kati ya
Ujerumani na Mexico.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Claudio Bravo aivusha Chile mbele ya Ureno, adaka penati 3 mfululizo"