


Mchakato wa Manchester United
kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 24, unasuasua baada ya
Real kupandisha dau la mchezaji huyo hadi karibu pauni milioni 80 (Mirror).
Morata ambaye ameoa hivi karibuni,
amelazimika kuondoka kwenye fungate yake ili kuharakisha uhamisho wake kwenda
Old Trafford (AS).
Wasiwasi kuhusu hatma ya Cristiano
Ronaldo unasababisha kuchelewa kutangazwa kwa uhamisho wa Alvaro Morata kutoka
Real Madrid kwenda Manchester United (Diario Gol).
Tottenham wapo tayari kumpa mkataba
mpya beki wake Toby Alderweireld, 28, ambaye ananyatiwa na Inter Milan (Daily
Mirror).
Mshambuliaji wa Sunderland Jermain
Defoe, 34, amekwama kwa sababu Bournemouth na West Ham zinachelea kumchukua
kutokana na gharama kubwa za mchezaji huyo (Daily Star).
Mshambuliaji wa Burnley Andre Gray,
26, anataka mkataba mpya wenye mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki, lakini klabu
hiyo inasema haina uwezo wa kumlipa (Daily Star).
Fernabahce ya Uturuki inafikiria
kupanda dau la kumchukua winga wa Everton Kevin Mirallas, 29 (Fanatik).
AC Milan wamejitoa katika mbio za
kutaka kumsajili kiungo wa Real Madrid, James Rodriguez, 25, na hivyo kuwapa
matumaini zaidi Chelsea na Manchester United (Mundo Deportivo).
Everton wamewazidi kete Manchester
United katika kumsajili beki Michael Keane, 24, kutoka Burnley na anatarajiwa
kutua Goodison Park siku chache zijazo (Sun).
AC Milan wanataka kumsajili beki wa
kati wa Arsenal, Laurent Koschielny, 31 (Telefoot).
Aston Villa watakamilisha usajili wa
beki John Terry, 34, wiki hii ambapo mkataba wake na Chelsea unamalizika (Daily
Mirror).
Manchester United bado wataendelea
kujaribu kumsajili kiungo wa Monaco Fanbinho, 23, licha ya kumchukua Nemanja
Matic, 28, kutoka Chelsea. Jose Mourinho huenda akamchezesha Fabinho kama beki
wa kulia (Independent).
Mshambuliaji wa Manchester United
Anthony Martial, 21, atamwambia Jose Mourinho kuwa anataka kuondoka, na klabu
hiyo haitamzuia kuondoka OT (Daily Express).
Manchester United wamepanda dau la
euro milioni 80 kumtaka kiungo wa Real Madrid James Rodriguez (Mediaset
Premium).
Francesco Totti, 40, anazungumza na
klabu ya Tokyo Verdy kuhusu mkataba wa pauni 50,000 kwa wiki. Totti anaondoka
Roma baada ya miaka 25 (Sun).
Barcelona wamejiwekea makataa ya
siku 10 wawe wamemsajili beki wa Arsenal Hector Bellerin na siku hizo zikipita
bila kumpata wataelekeza macho yao kwingineko (Mundo Deportivo).
Arsenal wana uhakika Alex
Oxlade-Chamberlain atasaini mkataba mpya wa pauni 100,000 kwa wiki, lakini
mchezaji huyo anataka kwanza kuhakikishiwa nafasi kabla ya kusaini (Evening
Standard).
Zinedine Zidane hana mpango wa
kumuuza Gareth Bale msimu huu, licha ya taarifa kuwa Real wanataka kumsajili
Kylian Mbappe (Marca).
Beki wa Chelsea Kurt Zouma, 22
huenda akajiunga na Nice kwa mkopo akisaka kucheza katika kikosi cha kwanza
(TalkSport).
Kurt Zouma au Michy Batshuayi, mmoja
wao huenda akauzwa Sevilla, kama sehemu ya mkataba wa Chelsea kumsajili winga
Vitolo (Express).
Manchester United wanataka kumsajili
kiungo wa Middlesbrough Marten de Roon, 26, na wanaamini anaweza kupatikana kwa
pauni milioni 8.8 (Tutto Mercato).
Chelsea, Tottenham, Everton,
Leicester, Southampton na Stoke, zote zinamtaka Ben Gibson, 24, lakini
watalazimika kulipa pauni milioni 25 kumpata beki huyo wa Middlesbrough (Daily
Star).
Tottenham wanamtaka beki wa
Southampton Cedric Soares, 25, lakini wanakabiliwa na upinzani kutoka Barcelona
na Juventus (Daily Mirror).
Kiungo wa Leicester Nampalys Mendy,
25, anataka kwenda Bordeaux baada ya kushindwa kucheza vizuri England
(L’Equipe).
Barcelona wamekasirishwa na nahodha
wao wa zamani Carlos Puyol, baada ya mmoja wa mabeki anaowawakilisha mwenye
umri wa miaka 16, Eric Garcia kuamua kuitosa Barcelona na kwenda Manchester
City (Independent).
Paris Saint-Germain wanajiandaa
kutoa euro milioni 240 kujaribu kuwashawishi Kylian Mbappe na kipa Gianluigi
Donnarumma. PSG watatoa euro milioni 135 kwa ajli ya Mbappe na euro milioni 39
kwa ajili ya kipa wa AC Milan Donnarumma, na pia wanataka kutoa euro milioni 42
kumtaka Fabinho wa Monaco na euro milioni 23 kumchukua Raphael Guerrerro kutoka
Borussia Dortmund (Sport).
Tianjin Quanjian ya China iko tayari
kurejea tena katika mbio za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund
Pierre Emerick-Aubameyang na wapo tayari kutoa euro milioni 80 (SportBild).
C&P S. Kikeke
Millionaire Ads
0 Comment untuk "TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATANO 28.06.2017"