Rasmi
timu ya Genk anayokipiga mtanzania Mbwana Ali Samatta haitakuwepo tena kwenye
mashindano makubwa ya Ulaya baada ya jana kukubali kichapo cha 3 - 1 kutoka kwa Oostende katika mchezo wa
mwisho ambao ndio ulikuwa unaamua timu ya kwenda Europa ligi hatua ya mtoani.
mchezo huo uliopigwa katika dimba la Versluys
Arena, Ostend. Magoli
ya Oostende yalifungwa na Akpala 27',Rozehnal
32' na Jali 51' wakati goli la Genk likifungwa na Schrijvers 45' kwa mkwaju wa
penati penati
baada ya Ruslan Malinovsky kukwatuliwa eneo la hatari.
Timu ya
Genk ilifika hatua hiyo baada ya kufunga timu ya Sint-Truiden V.V. katika
mchezo wa nusu fainali ya playoff ya kuwania kufuzu kwa hatua ya mtoano ya Europa
league kwa goli 3 – 0 ambapo Samatta alifunga goli la tatu.
katika mchezo wa jana Samatta alicheza dakika zote 90
katika mchezo wa jana Samatta alicheza dakika zote 90
Kwa Matokeo
hayo ya jana Genk itabidi isubiri msimu wa 2018/19 huenda wakapata nafasi ya
kurudi michuano mikubwa ya Ulaya.
video magoli yote ya mchezo huo >>>
0 Comment untuk "K.V. Oostende 3 – 1 K.R.C GENK, Ndoto ya Samatta kucheza michuano ya Ulaya yaota mbawa.videomagoli yote zipo"