Nahodha wa timu ya Simba Jonas Mkude
amesaini mkataba wa miaka miwili na kuondoa sintofahamu juu ya uwepo wake
katika timu hiyo ya Simba.
Ikumbukwe kuwa mkude alihusishwa
sana kuhamia timu ya Yanga lakini kwa sasa mambo yameisha ametia wino Msimbazi.
Wakati huohuo timu ya Singida United
inaonekana kujipanga vyema kwa ajili ya kuleta ushindani wa ligi kuu msimu ujao
baada ya kuinasa saini ya mfungaji bora wa nchi ya Rwanda kwa misimu miwili
mfululizo kutoka katika timu ya polisi ya Rwanda.
Danny Usengimana amesaini mkataba wa
miaka miwili.
0 Comment untuk " Mkude asaini miaka miwili ndani ya Simba, Singida United mmmmmh"