Tanzania
imepangwa kundi A pamoja na mataifa ya Mauritius, Malawi na Angola mataifa mengine yanashiriki michuano hiyo ya COSAFA ni Msumbiji, Shelisheli, Madagascar, Zimbabwe, Botswana,
Zambia, Afrika Kusini, Namibia, Lesotho na Swaziland.
Kwa
mujibu wa Mayanga, kikosi hicho kinaundwa na makipa Aishi Salum Manula
(Azam FC), Benno David Kakolanya (Young Africans SC) na Said Mohammed
Said (Mtibwa Sugar FC).
Walinzi
wa pembeni upande wa kulia ni Shomari Salum Kapombe (Azam FC)
na Hassan Hamis Ramadhan ‘Kessy’ (Young Africans SC) wakati upande wa kushoto
wapo Gadiel Michael (Azam FC) na Amim Abdulkarim (Toto Africans FC).
Walinzi
wa kati ni Erasto Nyoni (Azam FC), Salim Hassan Abdallah (Mtibwa Sugar),
Abdi Banda (Simba SC) na Nurdin Chona (Tanzania Prisons) wakati viungo wa
kuzuia kuwa ni Himid Mao (Azam FC) na Salmin Hoza wa Mbao FC.
Kadhalika
wako viungo wa kushambulia ambao ni Mzamiru Yassin Selembe (Simba), Simon
Happygod Msuva (Young Africans SC), Raphael Daudi (Mbeya City) na Shizza
Ramadhani Kichuya (Simba SC).
Katika
safu ya ushambuliaji wamo Thomas Emmanuel Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden),
Mbaraka Abeid Yusufu (Kagera Sugar), Stamili Mbonde, Elius Maguli (Dhofar SC)
na Shabani Idd Chilunda (Azam FC).
0 Comment untuk "Timu ya taifa itakayoshiriki COSAFA yatangazwa, vinara wa Yanga na Simba waachwa,"