TAARIFA KWA UMMA.
Klabu ya Yanga SC kupitia kwa Katibu
Mkuu Boniface Mkwasa inapenda kuwajulisha wanachama, wapenzi na washabiki wa
Yanga juu Mchezaji raia wa Rwanda Haruna Niyonzima ambaye amekua Mchezaji wetu
kwa misimu 6 mfululizo katika kiwango cha juu.Hata hivyo Haruna Niyonzima bado
ana mkataba mpaka mwezi Julai na Yanga Sc, lakini hatutaweza kuendelea kuwa nae
kwa msimu ujao kwani hatukuweza kufikia mwafaka katika mazungumzo yetu na yeye
licha ya timu yetu kuwa na nia za kuendelea nae kwa misimu miwili ijayo.Klabu
inamtakia kila la kheri katika maisha yake na soka kwa ujumla.
Imetolewa na Idara ya Habari na
Maelezo Young Africans Sports club.
21-06-2017.
0 Comment untuk "Niyonzima aachwa Rasmi na Yanga"