Kesho jumapili july 2, 2017 Timu ya
Taifa ya Tanzania Taifa Stars inashuka Dimbani kuwania kutinga nusu fainali ya
COSAFA dhidi ya wenyeji wao Afrika Kusini, mchezo utakaoanza saa 12 jioni kwa
saa za Tanzania.
Stars imeingia Robofainali baada ya
kuongoza kundi kwa kujikusanyia jumla ya Pointi 5, na kuziacha timu za Angola,
Mauritius na Malawi zikirudi makwao.
Mchezo wa kesho ni kipimo tosha kwa
Stars Kuelekea kwenye mchezo wake wa kuwania kucheza fainali za Afrika kwa
wachezaji wanaocheza ligi za ndani ‘CHAN’ dhidi ya Rwanda 12/07/2017.
Wachezaji wa Tanzania wanaendelea
kuimarika siku hadi siku na kuanza kuleta matumaini kwa wapenda soka wa
Tanzania ambao wamekata tama na timu yao ya Taifa kwani kwa miaka nenda rudi
inasindikiza.
Huenda huu ukawa mwanzo mzuri kwa
soka letu, watanzania tuungane kuipa sapoti timu yetu ya Taifa huenda wachezaji
wakajituma ipasavyo na kuiletea sifa nchi yetu.
Faida za COSAFA zipo nyingi kwa wachezaji
wetu ikumbukwe hiki ni kipindi cha usajili, jitihada za wachezaji ndio neema
kwa taifa letu, huenda tukauza baadhi ya nyota wa timu ya yetu ya Taifa kwenda
kwenye vilabu vikubwa Afrika.
Mchezo mwingine utakuwa baina ya Swaziland
vs Zimbabwe saa 20:30
Kilalakheri Tanzania hapo kesho
mkumbuke mamilioni ya Watanzania tupo nyuma yenu.
0 Comment untuk "South Africa vs Tanzania 18:00,jumapili july 2, 2017 Mtoto hatumwi dukani kesho"