Ilikuwa Alhamisi Juni 29, 2017 Rais wa timu ya
Simba ndugu Evans Aveva na makamu wake ndugu Geoffrey E,Nyange alimaarufu ‘Kaburu’
walipandishwa mahakamani kusomewa mashtaka yanayowakabili.
Viongozi hao walisomewa mashtaka
matano ikiwemo kughushi nyaraka, kutakatisha fedha nk.
Aliekuwa kiongozi wa Simba kwa
kipindi cha nyuma Ismail Adden Rage alitoa ufafanuzi juu ya mstakabali wa Simba
endapo viongozi wanapatikana na jambo zito kama hilo kwa mujibu wa Katiba ya
Simba.
Ismail Adden Rage alisema “kitakachoendelea
ni kuitisha mkutano mkuu na kumchagua kiongozi ambae amehudumu kwa muda mrefu
ndani ya kilab ‘Senior’ ndie atapewa jukumu la kuiongoza timu”.
Katiba hiyo inaonya kama viongozi
watatiwa hatiani basi watakuwa wamepoteza sifa za kuiongoza Simba.
“Huruhusiwi tena kuwa kiongozi
katika klabu yoyote ile, vilabu vya mpira vyote vimesajiliwa kwa msajili wa
vyama vya michezo, mimi binafsi nimewahi kupata matatizo lakini kwa bahati
nzuri mahakama ya rufaa ilinisafisha. Kwa kuwa mahakama ya rufaa ilinisafisha,
basi kwa maana hiyo katika maisha yangu bado sijawahi kutiwa doa mahali
popote.”
“Kwa bahati mbaya ikitokea
wakatiwa hatiani, lazima wakate rufaa waombe kusafishwa lakini kama wenyewe
wataridhikabasi hawawezi kuwa viongozi tena wa michezo kwa sababu sheria za
nchi wala katiba ya Simba haziruhusu.”Alisema Rage
Leo jumamosi mkutano umeitishwa
kwa lengo la kujadili na kujua mustakabali wa timu ya Simba barua inajieleza
hapo chini
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Uongozi wa simba kukutana leo kujadili mustakabali wa viongozi wao na kupitia katiba"