Mabingwa wa Afrika Timu ya taifa ya
Cameroon imeondoshwa rasmi katika michuano ya kombe la Mabara baada ya kupokea
kipigo cha goli 3 – 1 toka kwa mabingwa wa Dunia timu ya taifa ya Ujerumani.
Magoli yote manne yamefungwa kipindi
cha pili, Ujerumani ndio walianza kufungua ukurasa wa magoli mnamo dakika ya 48
pale
Dakika ya 64 ya mchezo mchezaji Ernest
Mabouka wa Cameroon alipewa kadi nyekundu Kutokana na mchezo mbaya alioucheza.
Dakika 67 na 82 Ujerumani walipata
goli la pili na la tatu kupitia kwa Timo Werner,
huku lile la kufutia machozi
la Cameroon likifungwa na
Vincent Aboubakar dakika ya 79.
Kwa Matokeo hayo timu za Cameroon na
Australia zinarudi makwao na kuziacha Ujerumani na Chile zikienda Nusu fainali.
Cameroon wameaga mashindano wakiwa
wa mwisho katika kundi B kwa kuambulia pointi 1 tu, wakati Australia wao wakiwa
na pointi 2.
Ujerumani ndio kinara wa kundi B kwa
kujikusanyia pointi 7 wakati Chile wanapointi 5 .
Nusu fainali ya kwanza itakuwa tarehe
28/06/2017 kati ya Portugal vs Chile
Nusu fainali ya pili itchezwa Tarehe
29/06/2017 kati ya Germany vs Mexico
0 Comment untuk "Ujerumani 3 – 1 Cameroon, Ujerumani yatinga Nusu fainali kombe la Mabara."