Meneja wa Manchester City Pep
Guardiola anataka kusajili mabeki wanne wapya – Dani Alves, 34, kutoka
Juventus, Kyle Walker, 27, kutoka Tottenham, Ryan Bertrand, 27, kutoka
Southampton na Benjamin Mendy, 22, kutoka Monaco (Star on Sunday).
Wanasheria wa Cristiano Ronaldo
wanadai kuwa mshambuliaji huyo wa Real Madrid, alilipa kodi nyingi kupita kiasi
kwa mamlaka za Spain, na sio kidogo kama inavyodaiwa (Cadena Cope).
Manchester United wamempa mkataba
wenye thamani ya euro milioni 7.5 kwa msimu, kiungo wa Roma
Radja Nainggolan (Il Tempo).
Liverpool wanataka kuongeza kasi
zaidi kwa kumtaka Alex Oxlade-Chamberlain wa Arsenal baada ya kukamilisha
usajili wa Mohamed Salah (Mirror).
Jose Mourinho ameitaka Manchester
United “kuvunja benki” na kutoa pauni milioni 100 ili kumsajili mshambuliaji wa
Tottenham Harry Kane na kuachana na Cristiano Ronaldo (Sunday Mirror).
Arsenal watamgeukia Anthony Martial
wa Manchester United iwapo watashindwa kumsajili Kylian Mbappe kutoka Monaco
(Mail Online).
West Ham wanajiandaa kutoa dau la
pauni milioni 25 kumtaka mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott (Daily Mirror).
Liverpool hawataki kukata tamaa ya
kumsajili Virgil van Dijk na wameambiwa na Southampton kuwa beki huyo
atagharimu pauni milioni 70 (The Express).
Real Madrid wamebadili mawazo yao ya
kutaka kumchukua Zlatan Ibrahimovic kwa mkataba wa muda mfupi (Don Balon).
Chelsea wapo tayari kuwapa Juventus,
Cesar Azpilicueta, kama fedha peke yake hazitatosha ili kumsajili Alex Sandro
(Calciomercato).
Rafael Varane ameshawishiwa kubakia
Real Madrid, huku kukiwa na taarifa kuwa Manchester United inamnyatia (Marca).
Manchester United wanamtaka beki wa
Barcelona Jordi Alba, lakini wamekiri wenyewe kuwa itakuwa vigumu kumpata (The
Sun).
Inter Milan wamewaambia Juventus
kuwa wanaweza kumsajili, Ivan Perisic, ambaye anasakwa na Manchester United
(Tuttosport).
Dani Alves amejaribu kumshawishi
Paulo Dybala kwenda naye Manchester City (Corriere dello Sport).
Juventus watamruhusu Alex Sandro
kujiunga na Chelsea iwapo mchezaji mwenyewe ataomba kuondoka (Metro).
Kiungo wa Monaco Tiemoue Bakayoko
anajiandaa kufanya vipimo vya afya Chelsea wiki ijayo (Evening Standard).
Paris Saint-Germain wanajiandaa
kutoa dau la pauni milioni 60 kumtaka mshambuliaji wa Manchester City Sergio
Aguero (The Times).
Chelsea wapo tayari kumruhusu
mshambuliaji wake Loic Remy kuondoka kwa bei poa (The Sun).
Ross Barkley anataka kuondoka
Everton ili kupata muda zaidi wa kucheza, ili aweze kuingia katika kikosi cha
timu ya taifa ya England huku Kombe la Dunia likinukia (Sun).
Rais wa Lyon amesema Arsenal lazima
waongeze dau lao na kufikia pauni milioni 57 iwapo wanataka kumsajili Alexandre
Lacazette, 26 (L’Equipe).
Arsenal wameanza mazungumzo kuhusu
mkataba mpya na kiungo Alex Oxlade-Chamberlain, 23 (Sun).
Kiungo wa zamani wa Tottenham,
Paulinho, 28, amesema Barcelona wanataka kumsajili, lakini hana mpango wa
kuondoka Guangzhou Evergrande ya China (Globo).
Mshambuliaji wa Arsenal Chris
Willock, 19, anakaribia kujiunga na Benfica bila malipo yoyote (Sunday Mirror).
Bournemouth wanajiandaa kumsajili
beki wa Chelsea Nathan Ake, 22 kwa pauni milioni 20 (Sun).
Newcastle na Southampton wanataka
kumsajili beki wa Arsenal Calum Chambers, 22 (Evening Chronicle).
Valencia wanataka kumsajili kipa wa
akiba wa Arsenal Emiliano Martinez, na wapo tayari kutoa pauni milioni 5 (Sun).
Habari zilizothibitishwa tutakujuza
mara zitakapothibitishwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Tafadhali share
tetesi hizi na wapenda soka wote
C&P from Salim Kikeke
Millionaire Ads
0 Comment untuk "TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAPILI 25.06.2017"