Timu ya taifa ya Tanzania Taifa
Stars leo imeanza vyema mashindano ya COSAFA baada ya kuitandika bila huruma
timu ya Malawi kwa jumla ya goli 2 – 0.
Iliwachukua Stars dakika 13 baada ya
mchezo kuanza kuandika goli la kwanza likiwekwa wavuni na kiungo mshambuliaji
Shiza Kichuya.
Dakika tano badae yaani dakika ya 18
kichuya Tena aliuwahi mpira ambao ulikuwa unaelekea kwa mtu na kuukokota na
badae kupiga shuti la ufundi kwa kutumia mguu wake wa kushoto na kumshinda
mlinda mlango wa Malawi akiruka bila mafanikio.
Mpaka mapumziko ilikuwa 2 – 0.
Kipindi cha pili Malawi walionekana
kucheza zaidi kupitia upande wa kushoto lakini Gadiel Michael na Abdi Banda waliweza
kuwazua washambuliaji wa Malawi.
Maajabu ya leo ni mabadiliko
aliyofanya kocha wa Taifa Stars ya kuwatoa viungo washambuaji wote wawili na
kuingiza mabeki.
Alimtoa Kichuya akamuingiza Hassan
Kessy, akamtoa Msuva akamuingiza Chona.
Pia alimtoa mshambuliaji Elias
Maguri na kumuingiza ‘Samatta mpya’ MbarakYussuf ambae aliwasumbua atakavyo
mabeki wa Malawi.
Hadi mwisho wa mchezo Tanzania 2 – 0
Malawi.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Stars yafanya kweli South Afrika, yaitungua Malawi 2 - 0"