Mabingwa
wa UEFA Champions league timu ya Real Madrid watakutana na vinara wa wa kombe
la vilab la kimataifa ICC timu ya Barcelona katika Elclassico ya kwanza tangu
kumalizika kwa msimu wa 2016/17.
Real Madrid
wanakutana na Barca bila nyota wake C. Ronaldo ambae alipewa mapumziko kufuatia
kuitumikia timu yake ya taifa ya Ureno katika michuano ya kombe la mabara.
Tukiangalia
timu ya Real Madrid:
Wachezaji
ambao wapo na timu nchini marekani ni
Makipa:
Navas, Casilla, Yanez, L. Zidane
Mabeki:
Carvajal, Ramos, Varane, Nacho, Marcelo, Theo, Quezada, Tejero, Achraf, Manu
Viungo:
Kroos, Casemiro, Modric, Isco, Ceballos, Kovacic, Oscar, Franchu
Washambuliaji:
Benzema, Bale, Vazquez, Gomez, Mayoral.
Hii ina
maana kama tutapanga kikosi kitakochaanza nadhani kitakuwa hivi: Navas;
Carvajal, Varane, Ramos, Marcelo; Modric, Casemiro, Kroos; Bale, Benzema, Isco.
Kwa kuangalia
kikosi hicho utaona kuwa endapo mabadiliko yatafanyika upande wa washambuliaji
nje kuna Mayoral na Vazquez.
Tuangalie
upande wa Barcelona:
Wachezaji
ambao wapo na timu nchini Marekani ni:
Makipa:
Cillessen, Ortola, Jokin
Mabeki:
Pique, Alba, Digne, Umtiti, Vidal, Marlon, Douglas, Vermaelen, Semedo
Viungo:
Busquets, Mascherano, Iniesta, Rakitic, Arda, D. Suarez, Roberto, Samper, Alena
Washambuliaji:
Messi, Neymar, L. Suarez, Alcacer, Munir.
Kikosi
ambacho tunafikiri kitaanza ni kama ifuatavyo: Cillessen; Semedo, Pique,
Umtiti, Alba; Rakitic, Busquets, Iniesta; Messi, L. Suarez, Neymar.
Kwa kuangalia
Barcelona utabaini asilimia kubwa wachezaji wao wapo na timu, hii ina mainisha
kuwa Barcelona wanaweza kuwa faida kubwa ya kushinda mchezo huo ila Real Madrid
na wao watataka kuonyesha kuwa bila Ronaldo wanaweza kuifunga Barcelona.
Mechi
itakuwa 50% 50% japo mashindano haya hayana sare ni lazima mshindi apatikane.
Kwenye
michuano hiyo Real Madrid ndio wanaburuza mkia baada ya kuambulia pointi 1
katika michezo 2 huku Barcelona wao wakiwa wanaongoza kituo hicho baada ya
kushinda michezo yao yote miwili na kufikisha pointi 6.
Huku Neymar
akiwa ndio anaongoza kwa kupachika magoli akiwa na goli 3
Siku ya
mchezo: 29/07/2017
Uwanja:
Hard Rock Stadium, Miami Gardens, Florida
Nchi:
Marekani
0 Comment untuk "ELCLASSICO KUPIGWA BILA RONALDO NCHINI MAREKANI, UCHAMBUZI NA UTABIRI"