Shirikisho la soka Duniani
limesitisha ujio wake nchini baada ya kupata taarifa ya kujitosheleza juu ya
kukamatwa kwa viongozi wa shirikisho la soka nchini Tanzania TFF.
Kaimu Rais wa TFF amekiambia chombo
kimoja cha habari asubuhi hii kuwa wamewaeleza FIFA kuwa viongozi hao
wameshikiliwa na serikali kwa makosa ambayo yanavunja Katiba ya nchi na wala
Serikali haijaingilia soka.
Pia TFF wameilithibishia Shirikisho
hilo kuwa mambo yapo shwari na serikali inafanya mambo yao kwa mujibu wa
sheria.
Leo kamati tendaji inakaa na
inategemewa kuja na tamko kuhusu uchaguzi mkuu wa TFF.
0 Comment untuk "EXCLUSIVE: FIFA wasitisha ujio wao nchini, wabariki kukamatwa kwa viongozi wa TFF"