Mshambuliaji mpya wa Simba, John Bocco ameongezwa katika
kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars.
Bocco amejumuishwa katika kikosi
hicho kufuatia kuumia kwa mshambuliaji Mbaraka Yusuph ambaye amekosa mechi
mbili zilizopita za Taifa Stars dhidi ya Mauritius na Afrika Kusini. Tayari
Bocco ameshajiunga na kambi ya Taifa Stars nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa mratibu wa taifa stars
Ahmed Mgoi amesema wapo katika taratibu za kumsajili Bocco ili aweze kutumika
katika michezo ijayo.
Mbarak yusuf jana alipelekwa Pritoria
hospitali baada ya kupata tatizo la kiafya.
Kesho Taifa Stars inacheza mchezo
mgumu dhidi ya timu ngumu ya Zambia katika hatua ya nusu Fainali.
0 Comment untuk "Bocco atua Afrika kusini, kurithi mikoba ya Mbaraka Yusuf"