Rais wa Simba na Makamo wake wamerudishwa
rumande hadi july 13, watuhumiwa hao wawili wanatuhumiwa kwa makosa matano
ikiwemo kutakatisha fedha na kughushi nyaraka.
Makosa matano yanayowakabili ni kama
ifuatavyo:
1. KUTAKATISHA FEDHA
Aveva alijipatia fedha kutoka
Barclays bank tawi la Mikocheni.
2. KUGHUSHI
Aveva alighushi nyaraka ili kujilipa
deni ambalo inadaiwa aliikopesha Simba USD 300,000.
3. KUTAKATISHA FEDHA KABURU
Kaburu alimsaidia Aveva kupata pesa
USD 300,000 kutoka Barclays Bank tawi la Mikocheni.
4. KUTAKATISHA FEDHA
Tarehe tofauti Aveva na Kaburu
walikula njama za kutakatisha fedha UDS 300000.
5. NYARAKA ZA UONGO
Walitumia nyaraka za uongo ili
kulipa deni kutoka benki ya CRDB.
Kwa mujibu ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kosa la utakatishaji fedha halina Dhamana hivyo watuhumiwa
wamerudishwa Rumande hadi july 13 kupisha upelelezi kukamilika.
Millionaire Ads
0 Comment untuk " Godfrey Nyange Kaburu na Evans Aveva Rumande mpaka july 13 2017"