Timu ya taifa ya Tanzania
imefanikiwa kutwaa nafasi ya tatu katika michuano ya COSAFA 2017, baada ya
kuitwanga Lesotho kwa jumla penati 4 kwa 2 baada ya dakika 90 kumalizika kwa
sare ya bila kufungana
Tanzania ndio wa kwanza kupiga
penati kupitia kwa Shiza Ramadhani Kichuya ambae alipga penati safi lakini
iligonga mwamba.
Penati zilizosalia za Tanzania
zilifungwa zote na wapigaji wakiwa ni Saimon Msuva, Himid Mao, Abd Banda na
Raphael Daudi.
Kipa wa Tanzania Said Mohamed ndie
aliekuwa shujaa baada ya kuokoa mkwaju mmoja na mkwaju mwingine ukigonga
mwamba.
Hongera Taifa Stars, Hongera
watanzania
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Hayawi hayawi yamekuwa Stars yawatoa kimasomaso watanzania, yatwaa nafasi ya 3 COSAFA"