Paris
Saint_Germain wana uhakika wa kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 198 wa
Neymar, 25, kutoka Barcelona katika siku 15 zijazo. (L’Equipe)
Barcelona
watajaribu kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, iwapo
watampoteza Neymar anayedhaniwa kuelekea PSG. (TalkSport)
Philippe
Coutinho ameiomba Liverpool ruhusa ya kuondoka, na tayari amefikia makubaliano
ya maslahi binafsi na Barca. (RAC1)
Barcelona
watawapa Liverpool kiungo Ivan Rakitic kama sehemu ya mkataba wa kumchukua
Philippe Coutinho. (Don Balon)
Hatua ya Real
Madrid kutaka kumsajili mshambuliaji wa Monaco, Kylian Mbappe, 18, huenda
ikasababisha winga Gareth Bale, 28, kwenda Old Trafford. (Indepenent)
Meneja wa
Manchester City Pep Guardiola amesema klabu yake ina fedha za kutosha za
kupambana na Real Madrid katika kumsajili Kylian Mbappe. (Mail)
Meneja wa
Manchester United Jose Mourinho ameonesha dalili kubwa kuwa Zlatan Ibrahimovic,
35, atasaini mkataba kubakia Old Trafford. (Times)
Manchester
United wanajiandaa kutoa dau la pauni milioni 44.6 kumtaka mchezaji wa RB
Leipzig Emil Forsberg. (Daily Star)
Iwapo Kylian
Mbappe atasaini kwenda Real Madrid, Manchester United watataka kumsajili Gareth
Bale, huku taarifa kutoka Old Trafford zikisema kuna ‘nafasi kubwa’ ya Bale
kwenda Old Trafford. (The Independent)
Manchester
United bado wanataka kumsajili kiungo wa Chelsea, Nemanja Matic, 28, na
wanaamini wataweza kuwashawishi Chelsea kuwauzia kwa zaidi ya pauni milioni 40.
(Independent)
Licha ya
kuhusishwa na kuhamia Manchester United, Ivan Perisic atapewa mkataba mpya
kubakia Inter Milan, ambao hawaamini Man Utd watakubali kutoa fedha zaidi na
kukubali mkataba ambao utamhusisha Anthony Martial kwenda Inter. (Football
Italia)
Manchester United
watamgeukia Emil Forsberg wa RB Leipzig iwapo watamkosa Ivan Perisic.
(Calciomercato)
Gareth Bale
amekataa nafasi ya kuhamia Arsenal, ambao wanamtaka ili kuziba nafasi ya Alexis
Sanchez. (Don Balon)
Kiungo wa
Arsenal Jack Wilshere, 25, anataka kubakia England iwapo ataondoka Emirates.
(ESPN)
Arsenal
wanakaribia kukamilisha usajili wa pauni milioni 45 wa kiungo wa Monaco Thomas
Lemar. (Sun)
Thomas Lemar
huenda akabakia Monaco, baada ya makamu wa rais wa klabu hiyo Vadim Vasilyev
kusema kiungo huyo hauzwi. (Metro)
Arsenal
watamkosa kiungo wa Barcelona Arda Turan, huku Galatasaray ya Uturuki
ikikaribia kukamilisha usajili wake. (Mirror)
Kiungo wa
Borussia Dortmund Mikel Merino, 21, anakaribia kujiunga na Newcastle. (Evening
Chronicle)
Beki wa kati
Mamadou Sakho, 27, hajajumuishwa kwenye kikosi cha Liverpool cha wachezaji 30
watakaocheza mechi tatu za kirafiki nchini Ujerumani. (Liverpool Echo)
Chelsea
wanataka kukopa pauni milioni 500 ili kujenga uwanja wao mpya, badala ya
kutegemea fedha za Roman Abramovic. (Times)
Chelsea
wanazungumza na wadau mbalimbali kuhusu uuzaji wa haki za jina la uwanja mpya,
ingawa klabu hiyo inasisitiza kuwa jina la Stamford Bridge litapewa heshima
yake kwa njia moja ama nyingine. (Evening Standard)
Meneja wa
Chelsea Antonio Conte amesema angepewa nafasi ya kununua mshambuliaji yoyote
yule duniani angemnunua Harry Kane, 23, wa Tottenham. (Daily Mail)
AC Milan
wamekuwa na mawasiliano na wakala wa Diego Costa kutaka kumsajili mshambuliaji
huyo wa Chelsea. (Daily Express)
Wakurugenzi
wakuu wa AC Milan Marco Fassone na Massimo Mirabelli wamekutana na wakala Jorge
Mendes kumzungumzia Cristiano Ronaldo. Vigogo hao wa Milan wanataka wajulishwe
mara tu Ronaldo atakapoweza kupatikana ingawa hakuna majadiliano yoyote kwa
sasa. (Sky Sports)
Tottenham
wanamnyatia kiungo wa Benfica Ljubomir Fejsa, 28. (Sun)
Meneja wa
Everton Ronald Koeman anataka kusajili wachezaji wengine watatu- beki wa kati,
mshambuliaji na kiungo mshambuliaji wa Swansea Gylfi Sigurdsson. (Mirror)
Millionaire Ads
0 Comment untuk " TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI 27 JULY,2017"