Mshambuliaji
mpya wa timu ya Difaa Hassan El Jadida ya Morocco, Mtanzania Ramadhani Singano
‘Messi’ juzi ameanza kuitumikia timu yake hiyo ilipokuwa inacheza mchezo wa
kirafiki na timu ya Olympic Club de Safi (OCS) katika mchezo wa kirafiki ambao
Aljadida walichezea kichapo cha goli 3 – 0.
Singano
amejiunga na Aljadida akitokea timu ya Azam baada ya mkataba wake kumalizika.
Ikumbukwe
na mtanzania mwingine Saimon Msuva atajiunga na timu hiyo na kufanya ndani ya
timu hiyo kuwa na wachezaji wawili wa Tanzania.
Pengine
huenda tukawaona mawinga hao wawili wakiwa kikosi cha kwanza kwenye michuano
mbalimbali ikiwemo ligi ya mabingwa Afrika.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "SINGANO AANZA KUITUMIKIA ALJADIDA:"