Alexandre
Lacazette amekamilisha vipimo vya afya Emirates na mkataba wake wa miaka mitano
wa pauni milioni 52 unatazamiwa kuthibitishwa baadaye leo (BBC, Sky).
Nahodha
wa Manchester United Wayne Rooney, 31, ameondolewa kwenye kikosi
kitakachosafiri kwenda Marekani, na atakamilisha uhamisho wake wa bila malipo
kurejea Everton mwishoni mwa wiki. Everton pia wanataka kumsajili Olivier
Giroud, 20, kutoka Arsenal kwa pauni milioni 20 (Sun).
Manchester
United wanataka kupanda dau jipya kumtaka winga wa Inter Milan Ivan Perisic, 28
(Sky Italia).
Manchester
United watafanya jaribio la mwisho kutaka kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid
Alvaro Morata, 24, wiki hii, huku Real wakigoma kushusha bei ya pauni milioni
72 (Independent).
Beki
wa Roma Antonio Rudiger, 24, amewasili London kukamilisha uhamisho wa pauni
milioni 36 kwenda Chelsea (Daily Mirror).
Chelsea
wanafikiria kumchukua pia kipa wa Paris Saint-Germain Alphonse Areola, 24
(Transfermarketweb).
Manchester
City wamekataa ombi la Newcastle United kumchukua kipa Joe Hart, 30, kwa mkopo
(Daily Mail).
Mshambuliaji
wa Monaco Kylian Mbappe, 18, ametoa sharti la kuwa mchezaji anayelipwa zaidi-
nyuma tu ya Cristiano Ronaldo- iwapo Real Madrid wanataka kumsajili (Diario
Gol).
Meneja
wa Leicester City ametoa dau la pauni milioni 20 kumtaka mshambuliaji wa
Watford Troy Deeney, 29 (Daily Mirror).
Tottenham
wanataka kumchukua kiungo wa Everton Ross Barkley, 23, lakini hawapo tayari
kulipa pauni milioni 50 wanazotaka Everton (Sun).
Liverpool
wametoa dau la pauni milioni 14.9 kutaka kumsajili beki wa Lyon Emanuel
Mammana, 21 (Sport Review).
Juventus
wamempa beki wao Alex Sandro, 26, mshahara wa pauni 84,000 kwa wiki ili
kumshawishi asiondoke kwenda Chelsea ambao wapo tayari kutoa pauni milioni 61
kumnunua (London Evening Standard).
Kiungo
wa Arsenal Santi Carzola, 32, ambaye hajacheza tangu Oktoba 2016, huenda
akakosa msimu ujao wote wa 2017/18 kutokana na kuwa majeruhi bado (Daily
Express).
Beki
wa Arsenal Hector Bellerin, 22, ameiambia klabu yake kuwa anataka kuondoka,
lakini meneja Arsene Wenger amekataa ombi lake la kutaka kuondoka. Barcelona
wanataka kumsajili beki huyo kwa pauni milioni 35 (Daily Express).
Tottenham
wanataka kumsajili Alfie Mawson, 23, kutoka Swansea, au Ben Gibson, 24, kutoka
Middlesbrough, huku wakitaka kumuuza beki wao wa kati Kevin Wimmer, 24 kwa
pauni milioni 20 (Daily Mirror).
Dau
la pauni milioni 8 kumsajili mshambuliaji Britt Assombalonga, 24, limekataliwa
na Nottingham Forest (Daily Mail).
Crystal
Palace wanafikiria kusajili mabeki wawili Joel Veltman, 25, na Kenny Tete, 21,
kutoka Ajax kwa pauni milioni 10 (Guardian)
Newcastle
wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa Burnley Andre Gray, 26 (Shie;ds Gazette).
Habari
zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya
wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Kwa mujibu
wa Salim Kikeke mtangazaji wa BBC
Millionaire Ads
0 Comment untuk " TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATANO 05.07.2017"