Ligi kuu ya England maarufu kama EPL
imeanza rasmi jana baada ya mabingwa wa FA na mabingwa wa ngao ya jamii timu ya
Arsenal kuendeleza ubabe dhidi ya vibonde wao kwenye ligi timu ya Leicester
City kwa kuidungua goli 4 – 3.
Alikuwa ni Alexandre Lacazette
dakika ya 2 aliwaamsha wapenzi na mashabiki wa Arsenal baada ya kuukwamisha
mpira wavuni kufuatia kazi nzuri ya Mohamed Elneny.
Shinji Okazaki alichomoa goli hilo
dakika ya baada ya Harry Maguire kufanya kazi ya zaa dakika ya 5.
Dakika ya 29 Jamie Vardy aliongeza
goli la pili
Danny Welbeck alifunga la pili mnano
dakika 3 za nyongeza za kipindi cha kwanza (45+3) akimalizia kazi kwa mchezaji
anaekuja kwa kasi Saed Kolasinac.
Mpaka mapumziko Arsenal 2 – 2 Leicester.
Kipindi cha pili Jamie Vardy alifunga
goli la tatu na la pili kwake dakika ya 56 mtengenezaji wa goli hilo alikuwa ni
Riyad Mahrez.
Magoli mawili ya Arsenal yalifungwa
na Aaron Ramsey na Olivier Giround
Mpaka mwisho wa mchezo Arsenal 4 – 3
Leicester.
Hivyo Arsenal wamendeza historia ya
vipigo pindi wanapokutana na Leicester kwani historia inaonyesha kuwa tangu
31/8/2014 arsenal ametoka sare michezo miwili tu na kushinda michezo yote
iliyobaki ya EPL.
Mechi yenye magoli mengi ni 5 -2
na 4 -3 idadi ikiwa magoli 7.
Takwimu kwa kifupi tangu 2014
31/8/2014 >>>>>Leicester
1 – 1 Arsenal
10/2/2015>>>>>Arsenal
2 - 1 Leicester
26/9/2015>>>> Leicester
2 – 5 Arsenal
14/2/2016>>>>>Arsenal
2 – Leicester
20/8/2016>>>> Leicester
0 – 0 Arsenal
26/4/2017>>>>Arsenal 1 –
0 Leicester
11/8/2017>>>>Arsenal 4 –
3 Leicester.
Kwa takwimu zilivyo hapo juu
utakubaliana na mimi kuwa Leicester ni kibonde wa Arsenal kwenye EPL.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Arsenal waendeleza ubabe kwa vibonde wao Leicester City epl, wainyuka 4 - 3"