Taarifa hiyo iliyotolewa jana iko
hivi:
*SIMBA SPORTS*
*DAR ES SALAAM*
*11-8-2017*
*DAR ES SALAAM*
*11-8-2017*
*TAARIFA KWA UMMA*
*_______________________________*
*_______________________________*
Klabu ya Simba inawatangazia
Wanachama wake na wadau wa mchezo wa kandanda kote nchini kuwa Mkutano wake
mkuu wa kawaida wa kila mwaka upo pale pale.
Hatua hiyo inafuatia na Hukumu
iliyosomwa leo katika Mahakama ya kisutu, kufuatia zuio la kuzuia Mkutano huo,
liliowekwa na mmoja wa wadhamini wa klabu Mzee Hamis kilomoni.
Kwenye hukumu hiyo,mahakama hiyo
ilitupilia mbali shauri hilo.
Mkutano huo utafanyika siku ya
Jumapili tarehe 13-8-2017, kuanzia saa Nne kamili asubuhi, ukitanguliwa kwa
Wanachama wa klabu kujiandikisha kuanzia saa mbili kamili asubuhi.
Klabu imeamua kufanyia mkutano
huo kwenye Ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyarere international
Conference Centre).
Ukumbi huo wa kisasa kabisa
nchini upo maeneo ya Ocean Road, jirani na Chuo cha Usimamizi wa fedha(IFM), Na
itakuwa mara ya kwanza kwa vilabu vya michezo nchini kufanyia mkutano wake
kwenye kituo hicho kilichobeba jina la Baba wa Taifa hili.
Uongozi wa Simba unawaomba
wanachama wake kuhudhuria kwa wingi kwenye mkutano huo muhimu,huku mahitaji
yote muhimu yakipatikana siku hiyo ikiwemo Vinywaji baridi na Chakula cha
mchana.
*Mwisho*
klabu inawaomba tena Wanachama
wake wenye hoja tofauti waje kuzitoa ndani ya Mkutano huo kama inavyoagiza
katiba ya klabu.
Hakika huu ni ushindi mkubwa sio
tu kwa klabu, bali kwa Mustakbali mzima wa maendeleo ya mchezo huu murua zaid
nchini na kote Ulimwenguni.
IMETOLEWA NA..
*HAJI S MANARA*
MKUU WA HABARI SIMBA SC
*SIMBA NGUVU MOJA*
0 Comment untuk "SIMBA IMETOA TAARIFA YA MKUTANO KESHO KAMA KAWA"