Mabingwa wa Tanzania siku ya
jumamosi na jumapili wataendelea na kutest mitambo yao kabla ya Tarehe 23
kukutana na watani zao wa jadi ambao pia ndio mabingwa wa kombe la Azam Sports
federation.
Yanga watacheza mchezo wa kwanza
siku ya jumamosi kwa kuwakabili Ruvu Shooting ya mkoani Pwani katika Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.
Na siku ya jumapili watacheza mchezo
mwingine katika ardhi ya Zanzibar ndani ya dimba la Aman dhidi ya wenyeji wao
timu ya Mlandege.
Baada ya kucheza na Mlandege Yanga watasafiri
hadi kisiwa cha Pemba kwa kambi ya maandalizi ya mchezo wa ngao ya jamii dhidi
ya Simba katika Uwanja wa Taifa Tarehe 23 August, hayo yaote yametolewa na katibu mkuu wa Yanga bwana Mkwasa
0 Comment untuk " Ratiba ya michezo ya Yanga kabla ya kukutana na Simba august 23"