Aliyekuwa rais wa zamani wa
Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) ambae pia ni raia wa Cameroon Issa
Hayatou ameibuka na kumshauri rais wa CAF bwana Ahmad kuangalia tena uamuzi
wake wakutaka kuinyang’anya Cameroon kuandaa michuano y mataifa ya Afrika mwaka
2009.
Hayatou amemsihi bosi huyo mpya wa
CAF kutembelea Cameroon na kujionea miundo mbinu ya viwanja inavyoendelea
“tumejenga viwanja vitano na kingine
kipo katika hatua nzuri yote hii ni kuhakikisha tunaandaa michuano hiyo ya
mwakani, pia kuna miaka miwili mbele mpaka 2019 hivyo asituhukumu sasa”alisema
Hayatou.
Hii imekuja baada ya Ahmad kutaka
kutangaza upya tenda kwa nchi ambayo itaweza kuandaa mashindano ya hayo ya
Afcon kwa kigezo kuwa Cameroon wanasua sua kwenye maandalizi.
0 Comment untuk "Hayatou Ang’aka Baada Ya Ahmad Kutaka Kuipokonya Camerron Uenyeji Afcon 2019"