Zikiwa zimesalia siku mbili pekee
kuelekea mchezo wa Watani katika Ngao ya Jamii Jumatano hii, mshambuliaji wa
Yanga Amissi Tambwe ameipiga mkwara Simba kwa kuwaambia haya:
“Namshukuru Mungu hivi sasa nipo
fiti na ninaendelea vizuri na maandalizi yangu kuelekea mchezo huo baada ya
kupona goti lililokuwa likinisumbua hivi karibuni.
“Ninamshukuru Mungu kwa kunijalia
afya njema na nipo tayari kwa ajili ya mechi ya Jumatano dhidi ya Simba, kwani
nimemisi sana kuifunga jambo ambalo linanifanya nijisikie vibaya kila wakati.
“Endapo nitapata nafasi ya kuanza
hiyo Jumatano dhidi ya Simba, nitahakikisha napambana vilivyo ili niweze
kuzifumania nyavu roho yangu itulie kwani nataka nizidi kuandika rekodi ya
kuifunga mara nyingi,”
Millionaire Ads
0 Comment untuk "TAMBWE AIPIGA BONGE LA MKWARA SIMBA"