Wanariadha 8 walioiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Dunia nchini
uingereza katika jiji la London wanrejea nchini wakiwa na medali moja tu ya
Shaba ambayo mtanzania Alphonce Simbu ndie aliyeitwaa siku chache zilizopita.
Jana watanzania wawili ilikuwa wakimbie kwenye hatua ya fainali
lakini alikimbia mwanariadha mmoja na kuambulia nafasi ya 13 hivyo kukosa
nafasi ya kutinga fainali zitakazo fanyika siku ya jumamosi august 12.
Mtanzania aliekimbia jana ni Emmanuel Ginik
Giniki baada ya mashindano alisema “kiukweli
mashindano yalikuwa ni magumu na niliweza kujitahidi kwa kadri nilivyoweza
lakini kwa bahati mbaya kabsa kilichonitokea nilikuja kukanyangwa mguu
ilipobbaki mita 800 sasa nilishindwa kushindana kwa ile hali ya kupiga kiki
ndio ikawa sio bahati yangu tena”
Katibu alimpongeza Giniki kwa kumaliza mbio
“ujuzi ndio uliomuangusha Ginik na kujikuta kaingia kwenye boksi na
kushindwa kutoka na ndio pale akakanyangwa, lakini nampongeza sana kwa kumalizwa
mbio”alisema Gidabudai
“nimepata kuona maono ya Filibert Bay akimtabiria Ginik kuwa
atatumia dakika 13 na kuvunja rekodi ya taifa”aliendelea kusema.
Kuhusu mwanariadha Gabriel Gerald Gea ambae alitakiwa kukimbia mbio
hizo lakini hakuonekana gidabudai
alisema “Gea alikuwa akimbie na aliwekwa kwenye hit no two lakini hakuanza
mbio kwa sababu ya msituko wa
goti,makocha wawili na mimi tulikaa kulipeleka tatizo lake kwa madaktari ambao
wapo na jana waliamua kuwa Gea hatoweza kukimbia”
0 Comment untuk "WANARIADHA WA TANZANIA KAZI IMEISHA JANA USIKU SASA KUREJEA TANZANIA"