Kamati
ya nidhamu ya TFF jana August 31, 2017 ilitangaza kumuandikia barua ya onyo
kali winga wa Taifa Stars na klabu ya Difaa El Jadid ya Morocco Simon Msuva baada
ya kumkuta na hatia ya kumsukuma mwamuzi kwenye mechi ya mwisho ya ligi kuu
Tanzania bara msimu uliopita kati ya Mbao FC dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa
CCM Kirumba, Mwanza.
Sakata
hilo liliwahusu wachezaji watatu ambao awali walikuwa wanaitumikia timu ya
Yanga ambao ni Obrey Chirwa na Deus Kaseke Pamoja na Simon Msuva, lakini kwa
sasa aliyebaki Yanga ni Chirwa peke yake wakati Kaseke akisajiliwa na Singida
Utd na Msuva akijiunga na Difaa El Jadid ya Morocco.
Msuva
baada ya kukutwa na hatia aliomba radhi sana na kuwaasa wachezaji wengine wayaheshimu
maamuzi ya refa awapo uwanjani.
“Maamuzi
waliyotoa nayapokea kwa sababu hata kwa wachezaji wengine itawafundisha kwamba,
maamuzi anayotoa refa ndio hayohayo ameamua kutoa. Naomba radhi kwa
kilichotokea kwa sababu hakikutokea kwa pekeangu, tulikuwa wachezaji watatu
mimi, Chirwa na Kaseke, mimi naomba radhi na wao najua wataomba radhi kwa muda
wao,” alisema Simon Msuva.
0 Comment untuk "Msuva atoa neno baada ya kukutwa na Hatia ya kumsukuma "