Washambuliaji wa ligi kuu nchini Uingereza wanaonekana
hawataki mzaha msimu, na hili halipingiki miongoni mwa wadau wengi wa soka
ulimwenguni.
Chelsea wamemsajili Alvaro Morata kama mrithi wa Diego Costa
ambae kulitokea sintofahamu kati yake na kocha wa timu hiyo Conte hivyo
kulazimika kumpiga bei kwenda Atletico Madrid.
Ujio wa Morata watu waliubeza lakini kiwango alichokionyesha
mchezaji huyo tunaweza kusema dunia haiwezi kuhamaki mwisho wa msimu akiwa
mfungaji bora.
Kwanza amevunja rekodi ya Diego Costa ya kufunga magoli
matatu katika mchezo mmoja hat trick jana dhidi ya Stock City rekodi ambayo
iliwekwa na Costa tangu 2014 katika mchezo kati ya Chelsea na Swansea City.
Mpaka sasa ana goli 6 katika michezo sita ya ligi kuu nchini
Uingereza.
Lukaku anaendelea kuwathibitishia walimwengu kuwa thamani ya
euro milioni 75 ilikuwa sahihi kwake kama dau la uhamisho toka Everton kwenda
Man UTD.
Lukaku mapaka sasa ameshafunga magoli 6 katika michezo sita
ya ligi kuu nchini Uingereza.
Kama kawaida yake tayari ameshafunga goli 6 na nadhani msimu
huu kutokana na jinsi washambuliaji wa timu pinzani walivyo lazima afunge zaidi
ili kuiaminisha Dunia kuwa yeye bado yupo na kazi yake ni moja tu ya kucheka na
Nyavu
Baada ya vuta
ni kuvute ya kutakiwa na mzee Wenger kama mbadilishano na Sanchez Raheem
anaithibitishia dunia kuwa haikuwa sahihi kwake kutolewa yeye pamoja na pesa
kwa ajili ya dili la kumnasa Sanchez mpaka sasa amefunga goli 5.
Miongoni mwa
washambuliaji asili kwa sasa duniani ni pamoja na Vardy, Vardy mpaka sasa
amefunga magoli 5 na bado anaweza kuendelea kufunga nahii anauaminisha umma wa
wapenda soka kuwa yeye ni miongoni mwa washambuliaji bora kabisa kwa sasa
Huyu
ndie mfungaji bora wa msimu uliopita na kuna uwezekano akatetea kiatu chake
endapo atauendeleza moto alioanza nao mpaka sasa ana goli 4.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "TOP SCORES LIGI KUU UINGEREZA, MORATA, LUKAKU na AGUERO KAZI IPO MWAKA HUU"