Timu ya ndanda ya mkoani mtwara leo mchana imewatoa
hofu wadau na mashabiki wa timu hiyo popote pale walipo kuwa lazima Singida Utd
kesho waziachie pointi tatu ndani ya dimba la Nangwanda mjini Mtwara.
Akizungumza na waandishi wa habari Saidi Limbega
ambae ni mweka hazina wa Ndanda alisema “sisi kama timu tumejiandaa vizuri na
kikosi chetu kipo imara kwa mapambano ili kuweza kupata pointi tatu, tunahakika
ndanda ni wazuri zaidi ya Singida UTD,” “niwaombe wapenzi na mashabiki waje
watusapoti kwa sababu washangiliaji ni mchezaji wa 12 ” alisisitiza Limbega.
Limbega pia amesema baada ya mchezo huo timu itapata
mapumziko kwa siku mbili kabla ya maandalizi ya safari ya Bukoba kwa mchezo
ujao dhidi ya Kagera
Ndanda wapo nafasi ya 8 baada ya kucheza michezo 6 na kujikusanyia pointi 8.
Singida UTD wao wapo nafasi ya 5 wakiwa na pointi 11 baada ya michezo 6
Ndanda wapo nafasi ya 8 baada ya kucheza michezo 6 na kujikusanyia pointi 8.
Singida UTD wao wapo nafasi ya 5 wakiwa na pointi 11 baada ya michezo 6
0 Comment untuk "NDANDA WAAHIDI USHINDI MNONO SIKU YA KESHO DHIDI YA MATAJIRI SINGIDA UNITED"