Mabingwa watetezi wa
ligi kuu Tanzania Bara timu ya Yanga mchana huu wameelekea mkoani
Shinyanga wakitokea Tabora ambapo waliweka kambi ya muda kwa ajili ya
maandalizi ya mchezo dhidi ya Stand United.
Yanga wanaenda Kambarage wakiwa na kumbukumbu ya
kipigo cha golui 1 kwa 0 msimu uliopita katika uwanja huo.
Lilikuwa ni goli la
Pastory Atanas ambae kwa sasa anaitumikia timu ya Singida United ndio
lililoifanya Yanga msimu uliopita kuuona uwanja wa kambarage kuwa na mchungu
Hivyo mchezo wa Jumapili utakuwa mgumu kwa
timu zote mbili kwani Yanga wanataka kulipiza kisasi cha msimu uliopita na
kujiweka vizuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Stand United wanataka kupata ushindi ili
kujinasua mkiani kwani mpaka saa wana pointi nne huku wakiwa katika nafasi ya
15.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "YANGA IMEANZA SAFARI YA KUSAKA POINT TATU KAMBARAGE"