Timu ya taifa Ureno leo mida ya saa
nne kasorobo itakuwa na kibarua kigumu cha kupata tiketi ya moja kwa moja
kufuzu kombe la Dunia nchini urusi.
Ureno endapo watapata ushindi wowote
leo watakuwa wanawapiku vinara wa kundi hilo uongozi wa kundi kwa uwiano mzuri
wa magoli ya kufunga na kufungwa.
Mpaka sasa Switzerland wana pointi
27 wakati Ureno wana pointi 24.
Mpaka sasa Switzerland wamefunga
magoli 23 na wamefungwa magoli 5 wakati
Ureno imefunga magoli 30 na kufungwa magoli 4.
Hivyo ukiangalia takwimu hizo
zinambeba Ureno endapo atashinda mchezo huo.
Lakini Switzerland sio wakubeza
kwani katika mchezo wa Sep 6, 2016 walipata ushindi wa goli 2 – 0 mbele ya Ureno
kwa magoli ya Breel Embolo dakika 24 na Admir Mehmedi dakika 30 huku Granit
Xhaka akipewa kadi nyekundu dakika ya 90 na huo ulikuwa ni mchezo wa raundi ya
kwanza katika kundi.
Katika mchezo huo Ronaldo hakucheza
na huenda uwepo wake kwa siku ya leo ukaongeza kitu na Ureno kupata nafasi ya
moja kwa moja mbele ya mashabiki wake.
0 Comment untuk " RONALDO KUAMUA NAFASI YAO YA KUFUZU KOMBE LA DUNIA LEO MBELE YA VINARA SWITZERLAND"