Millionaire  Ads

Simba hii hatari sana, Yailaza Njombe 4, Okwi kama kawa, Mtibwa nayo ni Shida, Azam yabanwa mbavu




Simba walianza kwa kulisakama lango la Njombe ni uimara wa mlinda mlango wa Njombe ndio ulisaidia simba kuchelewa kupata goli mapema
Mnamo Dk 28, Okwi anaruka juu na kuunganisha vizuri kwa kichwa krosi ya Nyoni na kuiandikia Simba goli la kwanza.
Goli hilo lilidumu mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili Simba walikuja kwa ari na dakika Dk 51 pale Muzamiru alipounganisha krosi nzuri toka Emmanuel Okwi na kuandika bao safi na dakika mbili bado Mzamiru tena akafunga goli la pili kwake na la tatu kwa Simba huku majaro ikitoka tena kwa Okwi.  
Dk 60 krosi safi ya Kichuya , Mavugo anaunganisha kwa kichwa na kuwa bao la nne
Mpaka mwisho Simba 4 – 0 Njombe Mji
Kwa ushindi huo Simba inaendelea kubaki kileleni kwa idadi kubwa ya mabao iliyovuna msimu huu.
Matokeo mengine:
Lipuli 1 – 0 majimaji
Ndanda 0 – 0 Singida United
Mbao FC 0 – 0 Azam FC
Mtibwa 1 – 0 Prisons

Mbeya City 2 – 0 Ruvu Shooting
Millionaire  Ads

Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comment untuk "Simba hii hatari sana, Yailaza Njombe 4, Okwi kama kawa, Mtibwa nayo ni Shida, Azam yabanwa mbavu"

Back To Top