Mpaka sasa
timu zote barani Ulaya zimebakisha mchezo mmoja mmoja ili kumaliza mchujo wa kupata timu ambazo zitafuzu moja kwa
moja kwa kombe la Dunia nchini Urusi mwakani.
Kuna baadhi ya makundi tayari mambo yameshaeleweka
lakini kuna makundi mengine ambayo bado ngoma ni mbichi mpaka mchezo wa mwisho
ndio hatima ya nani anaenda Urusi na nani atacheza mchezo wa mtoano yaani Play
OFF.
Katika makala hii tutapitia makundi yote kuanzia
kundi A – I
Tukianza
kundi A.
Bado haijajulikana nani atapata tiketi ya moja kwa
moja angalia Msimamo kwenye kundi hapo juu.
Ufaransa anaongoza kundi A kwa pointi 1 mbele ya
Sweeden hii inategemea na mchezo wa mwisho ambapo kwa ufaransa ni ushindi tu
ndio utawahakikishia tiketi bila kujali Matokeo ya timu nyingine.
Michezo ya mwisho kwa kundi hili itapigwa mapema Tarehe
na muda kama unavyoonekana hapo chini
Kundi B.
Kundi hili tayari timu mbili za juu zishajitenga
ikimainisha kinara wa ligi ambae anahitaji pointi moja tu ili aweze kwenda
Urusi mwakani wakati Ureno ya Ronaldo bado inanyatia nyatia huku ikiiombea dua
mbaya Switzerland ifungwe kwa kuwa Ureno ina mtaji mzuri wa magoli ya kufunga
na kufungwa.
Mechi za mwisho zitakuwa kama ifuatavyo hapo chini:
kundi C:
Timu ya Ujerumani tayari imefuzu kabla ya kucheza
mchezo wa mwisho wakati huohuo Ireland kaskazini nayo imefuzu kwa hatua ya
mtoano Play Off.
Michezo ya mwisho itakuwa kama hivi:
kundi D:
Timu tatu za juu zote zinanafasi ya kupata tiketi ya
kwenda urusi mojamoja inategemea na jinsi zitakavyo zichanga karata zake siku
ya mwisho.
Hili ndio kundi pekee ambalo inawezekana kinara
akashindwa kufuzu na akakosa hata Play Off
Michezo ya mwisho itakuwa hivi:
kundi E:
Kundi hili timu tatu za juu zina nafasi sawa ya
kucheza play Off lakini Montenegro yenyewe imeshajitoa katika mbio za kuwania
nafasi ya moja kwa moja na kuziachia timu mbili za juu.
Japo Poland wana asilimia kubwa ya kufuzu licha ya
amsha amsha ya Denmark.
Ila Kutokana na mchezo wa mwisho endapo Montenegro
atashinda na Denmark akashinda kuna uwezekano mkubwa Poland akaishia nafasi ya
pili.
Michezo ya mwisho itakuwa kama hivi:
kundi F:
Kundi hili England tayari washafuzu imebakia nafasi
ya pili ambayo inagombewa na timu tatu kama inavyoonekana hapo juu.
Msimamo ulivyo Scotland lazima ashinde ili
ajihakikishie nafasi kinyume na hapo mambo yanaweza kugeuka.
Endapo atasuluhu halafu Slovakia akashinda kwa idadi
yoyote ya mabao basi safari ya Scotland itaishia hapo.
Michezo ya mwisho itapigwa leo majira ya saa moja
usiku na mpaka saa tatu tutajua ni taifa gani limefuzu kwa hatua ya mtoano
kundi G:
Kundi hili tayari lishafamika nani ni nani tayari
kama linavyoonekana kwa nafasi mbili za juu.
Watakamilisha Ratiba tu kwenye michezo ya mwisho:
kundi H:
Kundi hili nafasi inayogombaniwa ni nafasi ya pili
baada ya Ubeligiji kutwaa nafasi ya kwanza.
Timu iliyonafasi ya tatu na nafasi ya pili moja wapo
inaweza kutwaa nafasi ya pili.
Mechi za mwisho zitakuwa hivi:
kundi I
Hili nalo ni kundi la kifo na litaamuliwa na michezo
ya mwisho kila timu kuanzia nafasi ya tatu zina nafasi ya tiketi ya moja kwa
moja na kila timu ina nafasi ya kucheza play off ila na Uturuki nae endapo atashinda goli 9 kuna uwezekano nae akatinga nafasi ya pili.
0 Comment untuk "Ujerumani, Ubelgiji, Uingereza zimekata tiketi ya kombe la Dunia Ureno bado mambo magumu "