Timu ya taifa ya Tanzania Taifa
stars leo imejitutumua na kutoka sare ya goli moja kwa moja na wenyeji wao timu
ya Taifa ya Benin ‘The Squirrels’
Mchezo ulikuwa wa vuta nikuvute huku
Tanzania wakionekana wazuri eneo la katikati ambapo Mudathir Yahya na Hamisi
Abdallah walionekana kucheza vyema na kuzoena kwa haraka.
Benin ndio walikuwa wa kwanza kupata
goli kwa njia ya penati iliyoleta utata baada ya mchezaji mmoja wa Benin kuunawa
mpira na mwamuzi kuzani aleunawa alikuwa ni mchezji wa Stars.
Penati ilipigwa kiufundi na nahodha
wa Benin anaekipiga nchini Ufaransa katika ligi one katika kilabu ya Montpellier Stephane Sessegnon
Stars walienda mapumziko wakiwa
nyuma kwa goli .
Kipindi cha pili mchezo uli ‘balance’na
Tanzania iliweza kupata goli baada ya winga Shiza kichuya kupiga jaro moja kali
kutokea upande wa kushoto na Elius Maguli kuutumukiza wavuni mpira huo.
Hadi mwisho wa mchezo Benin 1- 1 Tanzani.
Kwa Matokeo haya Tanznia huenda
ikanufaika zaidi katika viwango vya FIFA kwa mwezi huu wa Novemba kwani Benin
ipo nafasi ya 77 wakati Tanznia ipo nafasi 136 na ukizingatia mchezo huu
umefanyika nchini Benin.
Tanzania iliwakilishwa na; Aishi
Manula, Himid Mao, Gardiel Michael, Abdi Banda, Kelvin Yondan, Hamisi
Abdallah/Jonas Mkude dk75, Simon Msuva/Boniphace Maganga dk85, Mudathir
Yahya/Nurdin dk92, Elias Maguli, Raphael Daudi/Mbaraka Yusuph dk54 na Shizza
Kichuya/Ibrahim Ajib dk65. Chona dk92, Elias Maguli, Raphael Daudi/Mbaraka
Yusuph dk54 na Shizza Kichuya/Ibrahim Ajib dk65.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "BENIN 1 - 1 TANZANIA, STARS BILA SAMATTA INAWEZEKANA WAIKAZIA BENIN NDANI YA NCHI YAO"