Matengenezo
Uwanja Mkuu wa Taifa, Dar es Salaam, umekamilika na Mheshimiwa Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison George Mwakyembe, ameambiwa
kuwa unaweza kuanza kutumika kuanzia Novemba 21, mwaka huu.
Kwa
msingi, Waziri Dk. Mwakyembe ametoa maagizo ya kuandaliwa mchezo maalumu
wikiendi ya Novemba 24, 25 au 26 kupata mchezo mmoja wa ufunguzi wa uwanja huo
wenye uwezo wa kubeba takribani mashabiki walioketi 60,000 kwa wakati mmoja.
Akipokea
ripoti hiyo kutoka kwa Alex – Mtaalamu kutoka Uingereza, Mheshimiwa Waziri Dk.
Mwakyembe amesema: “Tuna changamoto kwenye matunzo na matengenezo. Sasa ili
kukabiliana na changamoto hii, hatuna budi vijana sita waliofundishwa kazi na
mtaalamu huyu, wakafanyiwa mpango wa ajira. Vijana hao wavumilie kwa sasa”
Mtaalamu
huyo wa Uingereza, amesema kwamba wakati uwanja unatumika, ukarabati wa mara
kwa mara utakuwa ukiendelea ili kuifanya hazina hiyo ya taifa kuendelea
kuboreka kwa wakati wote.
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia akizungumzia
uboreshaji huo, alisema: “Ni vema wataalamu hao wakatumike pia kwenye viwanja
vya mikoani. Huko wataviboresha na kuwafundisha wengine.”
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Uwanja wa Taifa kufunguliwa Novemba 21, Mwakyembe ataka Mechi kali ya Ufunguzi"