Wachezaji wanaocheza ligi kuu bara
wameitwa kwenye kikosi cha wachezaji 30 wanaounda timu ya Taifa ya Zanzibar Zanzibar
heroes.
Wachezaji hao ambao wanacheza vilabu
tofauti wamejumuishwa na kocha wa timu hiyo kwa lengo la kuongeza ushindani wa
namba na wachezaji wanaocheza ligi ya Zanzibar.
Kocha wa timu hiyo Hemed Suleiman
'Morocco amewataja wachezaji hao kama ifuatavyo:
makipa; Ahmed
Ali ‘Salula’ (Taifa ya Jang’ombe), Nassor Mrisho (Okapi) na Mohammed
Abdulrahman ‘Wawesha’ (JKU).
Mabeki; Abdallah
Haji ‘Ninja’ (Yanga), Mohammed Othman Mmanga (Polisi), Ibrahim Mohammed
‘Sangula’ (Jang’ombe Boys), Adeyum Saleh ‘Machupa’ (Kagera Sugar), Haji Mwinyi
Ngwali (Yanga), Abubakar Ame ‘Luiz’ (Mlandege), Issa Haidar ‘Mwalala’ (JKU),
Abdulla Kheir ‘Sebo’ (Azam) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang’ombe).
Viungo; Abdul-Samad
Kassim (Miembeni City), Abdulaziz Makame (Taifa ya Jang’ombe), Mudathir Yahya
(Singida United), Omar Juma ‘Zimbwe’ (Chipukizi), Mohammed Issa ‘Banka’ (Mtibwa
Sugar), Amour Suleiman ‘Pwina’ (JKU), Mbarouk Marshed (Super Falcon), Ali Yahya
(Akademi ya Hispania), Hamad Mshamata (Chuoni) na Suleiman Kassim ‘Selembe’
(Majimaji).
Washambuliaji; Kassim
Suleiman (Prisons), Matteo Anthony (Yanga), Ali Badru (Taifa ya Jang’ombe),
Feisal Salum (JKU), Salum Songoro (KVZ), Khamis Mussa ‘Rais’ (Jang’ombe Boys),
Mwalimu Mohammed (Jamhuri) na
Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto).
Zanzibar inaenda kwenye mashindano
hayo ambayo mara ya mwisho kutwaa kombe hilo ilikuwa ni mwaka 1995 walipoifunga
Uganda kwenye mchezo wa fainali kwa goli moja kwa 0 goli likifungwa na Victor
Bambo.
Michuano ya challenge mwaka huu
itafanyika novemba 25 hadi disemba 9 nchini Kenya.
0 Comment untuk "Maproo ligi kuu Tanzania bara waitwa Zanzibar Heroes kwa ajili ya challenge"