Uzinduzi wa kamati hiyo ulifanyika
Ukumbi wa Watu Maalumu (VIP) katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ambako Mhe.
Waziri Dk. Mwakyembe alikubali kuwa Mwenyekiti wa Kamati huku Makamu Mwenyekiti
wake akiwa ni Rais wa Heshima wa TFF, Leodegar Chilla Tenga ilihali Mtendaji
Mkuu atakuwa Dk. Henry Tandau.
Wajumbe ni Makamu Rais wa TFF,
Michael Wambura na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda; Dk. Damas
Ndumbaro ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa za Leseni za Klabu ya TFF; Dk.
Francis Michael wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – Kitivo cha Sheria; Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Mohammed Enterprises, Mohammed Dewji na Mkurugenzi Mtendaji
wa Makampuni ya Said Salim Bakhressa, Abubakar Bakhressa.
Pia wamo Yussuph Singo Omari –
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo; Ahmed Msafiri Mgoyi – Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya TFF;
Khalid Abdallah – Mwenyekiti Kamati ya Maendeleo ya Vijana ya TFF kadhalika Dk.
Hamis Kigwangalla – Waziri wa Maliasili na Utalii.
Wajumbe wengine ni Nassib Mmbagga –
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke; Dar es Salaam; Angetile Osiah
Mhariri Mwandamizi wa Magazeti ya Kampuni ya Mwananchi Communications; Dk.
Allain Kijazi – Mkurugenzi Mkuu TANAPA; Dk. Dotto James – Katibu Mkuu, Wizara
ya Fedha na Mipango; Dk. A. P. Makakala – Kamishna Jenerali Idara ya Uhamiaji;
Dk. Fredy Manongi – Mkurugenzi Mkuu Hifadhi ya Ngorongoro.
Wamo pia Lameck Nyambaya – Mjumbe
Kamati ya Utendaji ya TFF; Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio; Kelvin Twissa
– Ofisa Masoko Mkuu Sportpesa; Profesa Lawrence Museru – Mkurugenzi Mkuu
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili; Injinia Ladislaus Matindi – Mkurugenzi
Mtendaji ATCL na Devotha Mdachi – Mkurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania.
Pamoja na Wajumbe hao, wengine
wanaoingia kwenye kwa nafasi zao katika Kamati hiyo ya maandalizi ni Rais wa
TFF na Katibu Mkuu wa TFF
0 Comment untuk "Kamati maandalizi U17,2019 yatajwa, Mo, Bakheresa, Makonda Ndani"