Mabingwa wa soka mkoa wa Mtwara timu
ya Silabu leo majira ya Asubhi imepata ajali ikiwa inaelekea mkoani pwani
kucheza mchezo wake wa awali wa kombe la Azam Sports Federation dhidi ya Kisarawe United ya mkoani pwani.
Ajali hiyo ambayo imetokea maeneo ya
Mchinga katika mkoa wa Lindi imesababisha majeruhi kwa wachezaji 12.
Msafara wa timu hiyo ulikuwa na
wachezaji 18, benchi la ufundi watu 5, na viongozi 3
Majeruhi wote wamelazwa katika
hospitali ya mkoa wa Lindi.
Mchezo kati ya timu hizo mbili ulikuwa umepangwa kufanyika kesho novemba 2 umeahirishwa mpaka hapo utakapo tajwa tena.
Rais wa TFF Wallace Karia ametuma
salamu za pole kwa Silabu na mkoa wa Mtwara
0 Comment untuk "SILABU WAPATA AJALI WAKIWA SAFARINI KUELEKEA MKOANI PWANI KUWAKABILI KISARAWE UTD"