Michuano ya kombe la Shirikisho
Tanzania inaanza rasmi kutimua vumbi kesho katika viwanja mbali nchini.
Michuano hiyo ambayo bingwa mtetezi
ni timu ya Simba itaanza hatua za awali siku ya kesho kwa timu sita kuvaana
kwenye viwanja tofauti.
Michezo ya kesho itakuwa kama
ifuatavyo:
Buseresere ya Geita vs Isako ya
Songwe
Usamala ya Simiyu vs Sahale All
Stars ya Tanga
Mchezo kati ya Kisarawe United ya
Pwani na Silabu ya Mtwara umeahirishwa hadi hapo baadaye utakapotangazwa tena
kwa sababu ya majeruhi ya wachezaji.
Baada ya michezo hiyo raundi ya
kwanza itaanza Novemba 7,8 na 9
TFF imeshalipa timu hizo sita na
kesho Tarehe 2 novemba itamalizana na timu zitakazoanzia raundi ya kwanza ili
kuondoa visingizio vya maandalizi.
Mshindi wa mashindano haya ndie
anaeiwakilisha nchi katika kombe la shirikisho barani Afrika.
Ratiba kamili ya michezo ya raundi
ya kwanza ni kama inavyoonekana hapo chini:
Millionaire Ads
0 Comment untuk "AZAM SPORTS FEDERATION CUP KUANZA KUTIMUA VUMBI KESHO"