Simba
imeendelea kutoa burudani kwa Washabiki wake wa mikoani baada ya jana kucheza
mchezo wa kirafiki mkoani Rukwa.
Katika
mchezo huo ambao kocha wa Simba anautumia kwa ajili ya kuangalia wachezaji wake
wa akiba, Simba imefanikiwa kushinda kwa goli 3- 1.
Mabao
ya Simba yamefungwa na kiungo Mohammed ‘Mo’ Ibrahim moja dakika ya 29 na
mshambuliaji Juma Luizo mawili dakika ya 47 na 92.
Matokeo
hayo ni salamu kwa mchezo wao ujao dhidi ya wajelajela timu ya Tanzania
Prinsons.
Simba
itaondoka Rukwa leo kwenda Mbeya kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo dhidi ya
Prisons.
Wachezaji
wa Simba kwa siku ya jana:
Emmanuel
Mseja/Ali Salim dk70, Ally Shomary, Jamal Mwambeleko/Nicholas Gyan dk60, James
Kotei, Yussuf Mlipili, Mwinyo Kazimoto, Jamal Mnyate, Muzamil Yassin, Juma
Luizo, Haruna Niyonzima na Mo Ibrahim.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Simba yatuma salamu kwa Tanzania prisons, yaitandika Kaengesa ya Sumbawanga goli 3 – 1, Luzio akiwa shujaa."