Singida UTD kwa mara ya kwanza
wakiwa kwenye Uwanja wao wa nyumbani jana walitoka sare ya bila kufungana na
mabingwa wa soka nchini timu ya Yanga.
Singida walionekana bora vipindi
vyote kwa aina yao ya uchezaji wa kutumia nguvu na kasi.
Dakika ya 54 Deus Kaseke
aliunganisha kwa kichwa mpira na kuingia ndani ya wavu kwa kupitia pembeni na
kuanza kushangila goli lakini umakini wa mwamuzi wa jana ndio ulioiokoa Yanga
kwani aliweza kuona kilichotokea.
uhodari wa mlinda mlango wa Yanga jana ulikuwa ni kigingi kwa Singida kwani aliweza kuokoa mashuti makali ya washambuliaji wa Singida wakiongozwa na Kutinyu
Mpaka mwisho wa mchezo Singida 0 – 0
Yanga
Kwa Matokeo haya Yanga imeendelea
kukamata nafasi ya pili nyuma ya vinara Azam Fc ambao wana pointi 19 baada ya
usiku wa jana kuifunga
Ruvu Shooting goli 1 kwa 0
Matokeo ya michezo mingine:
Ndanda 0 – 0 Mtbwa Sugar
Njombe mji 0- 0 Mbao FC
Kagera Sugar 0 – 0 Tanzania Prisons
Azam Football Club 1 – 0 Ruvu
Shooting
Msimamo upo hivi:
0 Comment untuk "Singida UTD waizindua Namfua kwa sare, Kaseke nusura aiangamize Yanga"