Timu ya taifa chini ya miaka 23
Kilimanjaro Warriors imetajwa jana na itaingia kambini kesho novemba 5
kujiwinda na michuano ya Cecafa Challenge Cup mapema mwezi December.
Kocha Msaidizi wa timu hizo, Oscar
Mirambo alitangaza majina hayo jana Novemba 03, mwaka huu huku akisema:
“Tunataka vijana wasiozidi 25 kwenye kikosi. Tutawapata kwenye kambi hii ya
siku 10 inayoanza tarehe 5, mwezi huu wa 11.”
Wachezaji aliowaita ni makipa
Metacha Mnata (Azam FC), Joseph Ilunda (JKT Ruvu), Liza Mwafwea (Tanzania
Prisons).
Wengine ni Cleotas Sospter (Yanga);
Idrissa Mohammed, Bakari Kijuji (Yanga), Joseph Prosper (Azam), Masoud Abdallah
(Azam), William (Ruvu Shooting), Yussuph Mhilu (Yanga), Adam Salamba (Stand
United), Omary Mponda (Ndanda) na Stanley Angeso (Stand United).
Pia wamo Eliud Ambokire (Mbeya City),
Emmanuel Kakuti (Mbeya City), Medson Mwakatunde (Mbeya City), Daruweshi
Shaliboko (Ashanti Unted), Abbas Kapombe (Azam/Ndanda), Ismail Aidan (Mtibwa
Sugar), Salum Kihimbwa (Mtibwa Sugar), Hassan Mganga (Mtibwa Sugar) na Award
Salum (Njombe Mji).
Wengine Awesu Ally (Mwadui), Salum
Chuku (Singida United), Yahya Zayd (Azam), Emmanuel Martin (Yanga), Geofrey
Mwashiuya (Yanga), Ayoub Masoud (Ndanda), Baraka Majogoro (Ndanda), Mohammed
Habib (Miembeni), Yussuf Mlipili (Simba), Agathon Mapunda (Njombe Mji), Faisal
Abdallah (JKU) na Yussuph Kagoma (Singida United).
0 Comment untuk "U-23 YATAJWA KUINGIA KAMBINI NOVEMBA 5 KUJIANDAA KWA MCHUJO WA KUPATA WACHEZAJI 25 WA CHALLENGE"