“Mata atakua mchezaji muhimu sana kwa Manchester United ya
Jose Mourinho” hayo ni baadhi ya maneno ya nguli wa soka Phill Nevile alipokua
anahojiwa na Sky Sports.
Neville ambae aliwahi kuwa nyota tegemeo la Man Utd miaka 90
na mwanzoni mwa 2000 aliendelea kusema “hapati majeraha hovyo, anatengeneza
nafasi nyingi za magoli, anacheza nafasi mbili au tatu uwanjani pia anafunga
magoli muhimu”
“nilihisi kua atakua mchezaji wa kwanza kufukuzwa na
Mourinho lakini ndio amekua mchezaji muhimu kwake”
Mourinho ndie aliemuuza Mata mapema January 2014 kwenda Man
Utd wakati huo chini David Moyes kwa kitita cha £37.1m.
Juan Mata ndie alieiwezesha Man Utd jana kuwafunga mahasimu
wao wakuu wa jijini la Manchester, Man city
katika mchezo wa EFL raundi ya 16 na kufanikiwa kutinga roba fainali ya
kombe hilo.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Phill Neville amtabiria makubwa Juan Mata ndani ya Old Traford"