Millionaire  Ads

manchester City 2 - 1 Swansea City: Gabriel Jesus arudisha Furaha Pep Guardiola, City yapaa hadi nafasi ya tatu


                                       Gabriel Jesus akifunga moja ya magoli ya leo
Etihad Stadium, Manchester
Manchester City imeitandika  Swansea City goli 2 -1 katika mchezo mkali na wakusisimua.
Kitu kizuri kwa Manchester city ni ujio wa mshambuliji Gabriel Jesus ambae ameongeza changamoto kwa Sergio Aguero katika nafasi ya upachikaji mabao.

Magoli yote miwili ya Manchester City yaliwekwa kimiani na Gabriel Jesus katika vipindi vyote viwili 11’ na 90’ wakati lile la kufutia machozi la Swansea limewekwa kimiani na Gylfi Sigurdsson 81’.

Mpaka mwisho wa mchezo huo Manchester City iliibuka na ushindi huo na kuiwezesha kufikisha pointi 49 nyuma ya Totenham yenye pointi 50 na chelsea yenye pointi 59.

Kadi za njano
 Manchester City:   Kevin de Bruyne 41’ na Raheem Sterling 44,
Swansea City : Fernando Llorente 60’ , Jack Cork 74’ na Gylfi Sigurdsson 90’
                                     possession (%)
Manchester City:  69
Swansea City:     31

Millionaire  Ads

Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comment untuk "manchester City 2 - 1 Swansea City: Gabriel Jesus arudisha Furaha Pep Guardiola, City yapaa hadi nafasi ya tatu"

Back To Top