KRC Genk leo inashuka katika dimba lake la nyumbani la
Luminus Arena kumenyana na timu inayoburuza mkia katika Belgium - Pro League timu
iitwayo Royal Excel Mouscron. Mchezo utakaopigwa saa 22:00 majira ya Afrka
Mashariki.
Cha kujivunia kwa watanzania ni mchezaji Mbwana Samatta
ambae anaiwakilisha vyema Tanzania kimataifa kwani mpka sasa yeye yupo nafasi
ya 15 pamoja na kiungo mshambuliaji wa Manchester City Kevin De Bruyne kwa
upachikaji mabao katika historia ya KRC Genk kwa kutia kambani jumla ya magoli
17 huku anaeongoza akiwa na magoli 105 ambae anaitwa Jelle Vossen.
Hii ina maana kuwa endapo Samatta atafunga goli tatu leo
atakuwa sawasawa na Christian Benteke ambae anakipiga katika klab ya Crystal
Palace.
Genk ipo nafasi ya 8 baada ya michezo 23 ikiwa na alama 34, huku kinara wa ligi hiyo Club Brugge ikiwa na alama 49 baada ya michezo 24.
Kilalakheri Samatta katika mafanikio yako Watanzania tupo
nyuma yako.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Samatta kibaruani leo Belgium - Pro League"