Palermo wapo mbioni
kumpa ulaji wa kuinoa timu hiyo Claudio Ranieri.
Rais wa kilabu ya Palermo
Paul Baccaglini anataka kumpa nafasi ya ukocha, aliyewahi kuwa kocha kwa
mafanikio makubwa na timu ya Leicester muitaliano Claudio Ranieri.
Palemo ambayo
inapigana kumbo kuepuka kushuka daraja msimu huu, inataka kumchukua Ranieri ili
aweze kuinusu timu hiyo na janga la kushuka daraja.
Rais huyo mpya anadhani
Ranieri ndio chaguo sahihi kwani alishawahi kuichezea timu hiyo hvyo anajuwa
mazingira ya Stadio Renzo Barbera.
Palermo ipo katika
nafasi ya 18 kati ya timu 20, ina pointi 15 katika michezo 29, katika michezo
yote hiyo Palemo imeshinda michezo matatu tu na kutoka sare michezo 6.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Ranieri apigiwa chapuo ukocha Palermo"