Unaweza kusema ulikuwa usiku mzuri
sana kwa Washabiki wa Arsenal na Simba ya Tanzania kwa kutwaa mataji kila timu
kwa ushindi unaofanana.
Dakika ya 4 tu Arsenal walianza
maandalizi ya kutwaa ya kombe hilo pale Alex Sanchez alipoiandikia timu yake
goli la kwanza baada ya beki wa Chelsea kukosea kuondosha mpira kwenye eneo la
hatari.
Dakika ya 57 na 68 Victor Moses wa Chelsea
alipewa kadi za njano ambazo zilisababisha apewe kadi nyekundu na kuifanya Chelsea
kucheza pungufu kwa dakika zilizobaki.
Dakika ya 76 Diego Costa
aliisawazishia Chelsea goli baada ya mbrazil Willian kupiga pasi safi langoni
mwa Arsenal.
Wenger alifanya badiliko la kiufundi
zaidi kwa kumtoa Danny Welbeck na kumuingiza Olivier Giroud katika dakika ya
78.
Mambo yaliiva pale fundi wa mpira na
asie na papara uwanjani Ozil pale alipomimina pasi safi na kutua kichwani mwa
Ramsey aliepiga kichwa cha kuogelea katika dakika ya 79 na kuipa timu ya
Arsenal taji la kwanza msimu huu mbele ya timu bora msimu huu na mabingwa wa
EPL Chelsea.
Takwimu za mchezo huo zinaonyesha
kuwa Arsenal walimiliki mpira kwa 52% zaidi ya Chelsea ambao wao walikuwa na
48%
Arsenal walitumia mfumo wa 3:4:2:1
Chelsea walitumia mfumo wa 3:4:3
Kwa Matokeo ya jana Arsenal sasa
ndio vinara wa kutwaa kombe la FA, wamelitwaa mara 13 na kuwaacha Manchester
United katika nafasi ya pili kwa kulitwaa mara 12.
Refarii: Anthony Taylor (England)
Watazamaji: 89472
Uwanja: Wembley
picha zaidi:
0 Comment untuk "Arsenal 2 – 1 Chelsea yatwaa kombe la FA mbele ya Chelsea, washabiki wa Arsenal roho kwatuuu"