Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania,
Salum Mayanga Jana Ijumaa Machi
19, 2017 ametangaza majina ya wachezaji 24 watakaounda kikosi cha Timu Tanzania
bara ‘Taifa Stars’.
Katika mkutano na wanahabari
uliofanyika Makao Makuu ya TFF, yaliyoko Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es
Salaam, Mayanga alisema kikosi hicho kinaundwa na
makipa :
Aishi Manula (Azam FC),
Benno Kakolanya (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).
Walinzi ni Shomari Kapombe (Azam FC) na Hassan Kessy
(Yanga SC) ,Mohammed Hussein (Simba) na Haji Mwinyi (Yanga SC), Erasto Nyoni (Azam FC), Salim Mbonde (Mtibwa
Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Aggrey Morris (Azam FC)
Viungo wa kuzuia kuwa ni
Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude (Simba SC).
viungo wa kushambulia Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC) na
Muzamiru Yassin (Simba) ,Simon Msuva (Yanga SC) na Shizza Kichuya (Simba SC),Farid
Mussa (Teneriffe, Hispania)
washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk- Ubelgiji), Thomas Ulimwengu (AFC
Eskilstuna – Sweden), Ibrahim Ajib (Simba SC), Mbaraka Yusufu (Kagera Sugar) na
Abdurahman Mussa (Ruvu Shooting).
Benchi la ufundi:
Mayanga (kocha mkuu), Novatus Fulgence (Kocha Msaidizi ), Patrick Mwangata (Kocha
wa Makipa), Danny Msangi( Meneja wa timu), Ally Ruvu (Mtunza Vifaa), Richard
Yomba (Daktari wa timu), Gilbert Kigadya (Daktari wa viungo).
Timu hiyo itaingia kambini May
23, 2017 kwenye Hoteli ya Urban Rose, Dar es Salaam mpaka tarehe 29 baada ya
hapo itasafiri kwenda Misri kwa kambi ya wiki moja kabla ya kurejea kuja
kucheza mchezo wa kufuzu Mataifa huru ya Afrika mchezo na Lesotho, mchezo
utachezwa Tarehe 10 mwezi wa 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
NB:Timu ya Taifa itakuwa chini ya
udhamini wa bia ya Serengeti.
0 Comment untuk "Kocha Mayanga Atajwa kikosi cha Taifa Stars, Kambi kuanza rasmi may 23, 2017"